Nguvu za kiume ni tukio pana sana lenye kuhusisha viungo na vitu vingi ndani ya mwili. Kuna zaidi ya viungo na vitu mbalimbali zaidi ya 100 ndani ya mwili wa mwanaume vinavyohusika na nguvu za kiume ambapo viungo hivi pia hufanya kazi zingine za mwili. Baadhi ya viungo hivyo ni ubongo, moyo, mishipa ya neva mishipa ya ateri, mirija iliyo ndani ya uume iitwayo corpora cavernosa.
Viungo vingine ni neva maalumu za parasympathetic, tezidume (prostate gland), ini, figo, homoni ya testestorone, kemikali za acetylcholine, serotonin, na dopamine, uti wa mgongo, eneo la chini ya mgongo (kiuno), eneo la nyonga.
Viungo vingine ni misuli maalumu iitwayo pelvic floor, tezi pituitari (pituitary gland), utando maalumu wa uumeni uitwao tunica albuginea, misuli iitwayo pubococcygeus [PC muscles], kemikali ya nitric oxide, kemikali ya prolactin n.k. Orodha ni ndefu sana, ni zaidi ya 100!
Unapopungua nguvu za kiume, kama nilivyosema hapo awali, ina maana ndani ya mwili wako kuna baadhi ya vitu katika vitu nilivyovitaja hapo juu havifanyi kazi vizuri jinsi ipasavyo. Yawezekana ni figo ndilo halifanyi kazi vizuri, au ini, au tezi dume, au neva ya parasympathetic, au moyo una tatizo au mishipa ya ateri, au misuli ya pelvic au homoni fulani iko juu sana au iko chini sana (hormonal imbalance), orodha ni ndefu sana. Kitendo cha baadhi ya viungo hivyo kutofanya kazi vizuri basi hapo hutokea upungufu katika nguvu za kiume. Upungufu huo unaweza kuwa ni:
1. Kukosa hamu ya mapenzi; au
2. Uume kusimama kwa uregevu; au
3. Kuwahi kufika kileleni; au
4. Kuchelewa sana kufika kileleni (au kushindwa kufika kileleni kabisa); au
5. Kushindwa kurudia tendo la ndoa; au
6. Kuhisi maumivu wakati wa tendo la ndoa au baada ya tendo hilo; au
7. Kukosa pumzi na uchangamfu wa mwili katika utendaji; au
8. Kuchoka sana baada ya tendo la ndoa na hata kukinai kabisa au hata kusikia kichefuchefu;
Ndugu msomaji, ili uelewe vizuri zaidi labda niseme kwamba, nguvu za kiume ni kiwanda; na ni zaidi ya kiwanda. Tukichukulia mfano wa kiwanda, ni kwamba ndani ya kiwanda kuna umeme, maji, madawa, watu (wafanyakazi wa kila taaluma na fani), mashine, mitambo n.k.
Ikitokea kitu kimojawapo kukosekana, mathalani umeme, au wafanyakazi wakagoma, au kukakosekana madawa muhimu au maji na kadhaa wakadha, basi bidhaa inayotarajiwa kupatikana sokoni, kwa hakika haitapatikana.
Vivyo hivyo nguvu za kiume, mathalani, ikitokea tezidume kutofanya kazi vyema, basi hapo mwanaume hatoona nguvu za kiume, zitapungua au zitaisha kabisa!
Kwa hiyo upungufu wa nguvu za kiume ni upungufu au kasoro za kiutendaji wa viungo ndani ya mwili wa mwanaume. Mwanaume yoyote anapaswa kutambua jambo hili, na siyo kukurupuka kubugia dawa tu.
MAELEZO ZAIDI BOFYA HAPA
No comments:
Post a Comment