Leo katika zama hizi za sayansi na teknolojia, tatizo la kupungua nguvu za kiume limekuwa kubwa sana, siyo Tanzania tu, bali duniani kote.
Hapo zamani, tatizo hili lilikuwa la wazee zaidi, lakini jambo la ajabu na la kuhuzunisha leo limekuwa ni tatizo la vijana zaidi kuliko hata wazee! Utamkuta mwanaume ni kijana wa miaka 18 au 25 au 30 au 40, lakini jinsi anavyotenda tendo la ndoa ni sawa na mzee wa miaka 90 au 100!!
Atakwambia, “Ninafika kileleni ndani ya dakika mbili,” au “Nikimaliza tendo la ndoa raundi ya kwanza, siwezi kurudia mpaka kesho yake!” Au “Uume wangu unasimama kwa uregevu sana, na nikiingia ukeni tu, unakufa (unaregea)!”
Habari kama hizo ni nyingi kwa namna tofauti tofauti na kwa watu wengi sana. Ni utitiri wa watu, vijana kwa wazee, na vijana ndiyo wakiwa wameshika usukani (wakiongoza).
Kwa bahati nzuri matatizo mengi ya nguvu za kiume yanatibika, lakini iwapo tu kama matibabu sahihi (yanayoanzia kwenye chanzo cha tatizo yatapatikana).
Hata hivyo, kwa bahati mbaya sana waathirika wengi wa nguvu za kiume wamekuwa wakikurupuka tu kubugia dawa, na hii ndiyo sababu wamekuwa hawaponi licha ya kutumia chungu ya dawa, na pia wamekuwa wakipoteza pesa nyingi bure tu kwa matibabu hayo ya kubahatisha.
Pia kutokana na tatizo hili kuwa kubwa, kila kuchapo huibuka watu wanaodai wanaweza kutibu na kumaliza tatizo kabisa. Kwenye magazeti, kwenye mabango mitaani, katika redio n.k, kuna utitiri wa matangazo juu ya tatizo hili. Lakini, kinachokata maini zaidi ni kwamba, wengi wa wataalamu hao hawajui sababu za kupungua nguvu za kiume, wala hawajui utendaji wa mwili wa binadamu. Wengi wanadhani kuishiwa au kupungua nguvu za kiume ndiyo ugonjwa wenyewe.
Kupungua nguvu za kiume siyo ugonjwa, ni dalili ya ugonjwa. Kuna sababu zake ndani ya mwili. Sababu hizo ni nyingi mno, ni zaidi ya 100! Anatakiwa daktari mtaalamu aliyebobea katika uzazi, mifumo ya mkojo, anayelijua vizuri figo ndani na nje, ini na mifumo mingine ya mwili, ikiwa ni pamoja na kemia ya mwili. Na inatakiwa dawa iende kutibu chanzo cha tatizo.
Jambo muhimu analopaswa mwanaume yeyote kufahamu ni kwamba, kupungua nguvu za kiume siyo ugonjwa, ni dalili ya ugonjwa. Sentensi hii ina maana gani? Twende pamoja.
SOMA ZAIDI HAPA
No comments:
Post a Comment