Tuesday, April 3, 2018

JE KITUNGUU SAUMU NI DAWA YA NGUVU ZA KIUME?

Kitunguu saumu
Baadhi ya watu wanadhani wanaweza kutibu upungufu wa nguvu za kiume kwa madawa ya kemikali kama vile Viagra n.k.

Hali hii imepelekea wanaume wengi kuendelea kupata shida ya upungufu wa nguvu za kiume kwa sababu ya kukosa kujua dawa sahihi ya nguvu za kiume.

​Ni ukweli usiopingika kwamba wanaume wengi tangu zamani za kale wamekuwa wakitibu nguvu za kiume kwa tiba asilia. Tiba ya asili ndiyo tiba bora kabisa ya kutibu upungufu wa nguvu za kiume, kwa sababu dawa hazina madhara kabisa.


Nguvu za kiume na vyakula


Naam! Ni sahihi na kweli kabisa kwamba kitunguu saumu kina msaada mkubwa katika nguvu za kiume. Lakini kuna kosa kubwa kwenye mitandao na hata madaktari na wagonjwa wenyewe. Kwa nini?

Kwa sababu mitandao inatoa ushauri wa jumla bila kuzingatia tatizo la mgonjwa. Upungufu wa nguvu za kiume una sababu nyingi sana. Na hivyo, si kila upungufu wa nguvu za kiume utatibiwa na kitunguu saumu. Ili unielewe vizuri tazama mifano hii mitatu hapa:

Abdi kapungukiwa nguvu za kiume kwa sababu figo zake hazifanyi kazi vyema.
Peter kupungua nguvu za kiume kwa sababu moyo wake haufanyi vyema kusukuma damu.
Samwel kapungukiwa nguvu za kiume kwa sababu ana tatizo katika tezidume
​Je, watu hao watatu utawapa ushauri wa kutumia kitunguu saumu?! Katika mitandao utakuta mtu kakopi na kupesti makala za watu kwamba tumia kitunguu saumu ni dawa ya upungufu wa nguvu za kiume, na hata wengine wamediriki kuiba makala zangu nyingi sana.

Na pia, kibaya zaidi maelezo juu ya namna ya kutumia vitunguu saumu hivyo hayajitoshelezi, na pia hata ni vitunguu saumu vya namna gani ni bora zaidi hawaelezi! Hali hii imewafanya watu wengi waendelee kuteseka sana.

Sasa turudi kwenye mada ya kitunguu saumu na nguvu za kiume na mfano wetu hapo juu. Kazi kubwa ya kitunguu saumu ni kusaidia mzunguko wa damu kutembea vyema na kufika mwilini kote katika kila kiungo. Kiambato kiitwacho allicin ndiyo kitu ambacho husababisha mtiririko wa damu kuongezeka.

Kama umepungukiwa nguvu za kiume kutokana na damu kutozunguka vizuri kwenda kwenye viungo vya mwili, basi kutumia kitunguu saumu ni jambo muafaka kabisa. Katika hiyo mifano yetu mitatu hapo juu utaona peter anaweza kupata msaada mkubwa wa kutatua tatizo lake la kupungua nguvu za kiume kupitia kitunguu saumu kwa sababu kitunguu saumu kimeenda kwenye tatizo husika kabisa. Lakini Abdi na Samwel wanaweza kumaliza miaka na miaka wasiweze kutatua matatizo yao. Kwa nini? Kwa sababu kuvimba kwa tezidume na figo kushindwa kufanya hakutibiwa na vitunguu saumu.

Kuhusu kiambato cha Allicin kilicho ndani ya kitunguu saumu


Allicin iligunduliwa na mtaalamu wa Kiitaliano wa Caribbean CJ Cavallito mnamo 1944, na ni mojawapo ya viambato muhimu viliomo ndani ya kitunguu saumu. Allicin kimsingi huwajibika kwa athari nyingi ikiwa ni pamoja na uwezo wake wa kuchangia matibabu ya shinikizo la damu na cholesterol ya juu, kukakamaa kwa mishipa au kuwa migumu (atherosclerosis), na kupungua kwa mishipa.

​Kutokana na ukweli kwamba atherosclerosis inachangia kupungua kwa mtiririko wa damu, ni sababu ya kuchangia upungufu wa nguvu za kiume, kwa mujibu wa madaktari wa moyo. Utafiti, hata hivyo, bado haujaweka moja kwa moja uhusiano kati ya allicini katika vitunguu na matibabu ya upungufu wa nguvu za kiume.

Wakati vitunguu inakabiliana na seli nyekundu za damu katika mwili, hidrojeni sulfudi, au H2S, huzalishwa. Watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Alabama huko Birmingham walichapisha utafiti katika jarida la Mahakama ya Taifa ya Sayansi mwaka 2007 ambayo ilionyesha kuwa H2S husababisha mishipa ya damu kutanuka na kupunguza shinikizo la damu na matatizo ya moyo.

Akiongoza utafiti, Dk David Kraus, Ph.D., aliripoti katika utafiti wake kwamba matokeo haya yanatoka katika polysulfides, ambavyo ni vitu vilivyo katika kitunguu saumu ambayo husaidia uzalishaji wa H2S.

​Uwezo wa vitunguu saumu wa kutanua mishipa ya damu huboresha mzunguko wa daumu, ambao kwa moja kwa moja huchangia kupunguza tatizo la upungufu wa nguvu za kiume. Ingawa matokeo haya yanatia moyo sana, utafiti zaidi unahitajika kuhusiana na uwezo wa kitunguu saumu katika kutibu upungufu wa nguvu za kiume.

KITAMBI KINAVYOATHIRI NGUVU ZA KIUME NA AFYA KWA UJUMLA

Madhara ya kitambi



Unajitazama katika kioo, lakini unachukizwa! Unachukizwa na mwili wako mwenyewe. Hauna la kufanya, unabaki kuhuzunika tu.

Tumbo! Tumbo!


Naam, tumbo lako linaonekana kutuna na kutengeneza mkunjo. Linaonekana kwamba linaweza kuchukua muda mrefu sana kuwa katika hali hiyo, inaweza kuwa miezi au miaka; au linaweza lisiishe kabisa!

Licha ya kuwa tumbo kubwa linaweza kuufanya mwili kuwa na muonekano mbaya usiopendeza, kwa hakika madhara yake kiafya ni makubwa zaidi kuliko ubaya wa sura yenyewe.

Katika lugha yetu ya Kiswahili, mafuta ya tumboni hujulikana kama “kitambi.” Lakini pia kuna majina mengi ya utani yanayotumika mtaani kukiita hicho kitambi, baadhi ya majina ni kama vile tumbo la mtungi, kishikio cha mapenzi, tairi la akiba, tumbo la bia, friji n.k.

Kwa nini watu walipachika majina kama hayo?

Katika miongo michache ya nyuma hapa kwetu Tanzania, na hata katika baadhi ya nchi duniani; baadhi ya watu kutokana ukosefu wa elimu walivitazama vitambi kama dalili ya ustawi mzuri wa maisha, na hasa ndiyo sababu ya kuvitengenezea majina ya ziada.

Katika miaka ya hivi karibuni, watu wengi sana sasa wametambua vizuri kuwa kitambi ni tatizo kubwa la kiafya. Utawaona wako katika kumbi za michezo ya mazoezi ya viungo (gym), wengine wakiwa katika utaratibu maalumu wa chakula (dieting); na wengine wakiwa katika programu za tiba ili kupunguza mafuta hayo mwilini, na ikiwezekana kuyaondoa yote kabisa.

Hata hivyo, wapo baadhi ya watu bado wanauchapa usingizi. Hao bado wanafanya utani na mafuta!

Ndani ya kitambi kuna nini?

Ukweli wa mambo ulivyo, kitambi hakina utani! Ukileta utani katika mafuta hayo ya tumboni, basi muda si mrefu utagonga hodi katika chumba cha daktari ukiwa tayari na kisukari (TYPE 2), au ugonjwa wa moyo, au kupooza, au saratani, au shinikizo la damu la kupanda (High Blood Pressure), au matatizo ya kibofunyongo, au ugonjwa wa ini (cirrhosis) huku kuishiwa nguvu za kiume ikiwa ni jambo linalokwenda bega kwa bega na kitambi.

Je, hapo utaendelea kufanya utani na kitambi? Bado utaita tumbo la bia? Au kadha wa kadhaa? Hakika utakiita ni tumbo la kifo!

Hayo siyo mafuta mazuri kabisa, wala siyo mafuta ya kuyatania wala kuyachekelea! Ukiyafungulia mlango tu na kuyaruhusu yaweke maskani yake tumboni mwako, ni sawa na kuruhusu nyoka kukaa chumbani mwako, hatima yake ni nini? Bila shaka ni kung’atwa! Kama zisipofanyika juhudi za haraka za kuidhibiti sumu ya nyoka huyo, basi matokeo yaweza kuwa kifo! Kitambi pia, ni vivyo hivyo.

Wakati mafuta mengi yanapokuwa mwilini huleta tatizo. Lakini mafuta haya ya tumboni yana hatari kubwa zaidi hata kama ni madogo.

Baadhi ya watu kwa kutojua madhara ya vitambi, huchukulia mambo kwa wepesi, husema, “Tumbo langu ni dogo tu, ni kama halipo vile!”

Kwa mtazamo wao, ni kwamba wanaweza kunusurika na madhara ya kitambi.

Ni kweli kwamba, watu wanatofautiana ukubwa wa matumbo. Kuna ambao matumbo yao ni madogo, au ndio yanaanza. Kuna wengine ni makubwa kiasi, na wengine makubwa zaidi kiasi ambacho huwafanya kupata taabu sana katika kufanya kazi mbalimbali.

Lakini, ukweli wa mambo ulivyo ni kwamba, mafuta ya tumboni yanaweza kukuletea maradhi hata kama hauna uzito mkubwa au hauna tumbo kubwa.

Kwa nini mafuta ya tumboni yalete maradhi? Yana uhusiano gani na maradhi? Kwa nini yapunguze nguvu za kiume? Haya ni baadhi ya maswali ambayo yanaweza kugonga katika akili ya msomaji.

Ukweli ni kwamba, tumbo kubwa ni matokeo ya mafuta mengi mno yaliyoweka makazi yake ndani kabisa ya tumbo au fumbatio (abdomen) na kitabibu yanajulikana kama, “visceral fat.” Mafuta hayo huzonga na kudhuru figo zako, ini na viungo vingine vilivyo tumboni na kuharibu utendaji wa kazi wa viungo hivyo na kuvuruga utendaji wa homoni.

Ni mafuta ambayo huleta madhara makubwa katika mishipa yako ya damu. Seli za mafuta hayo huzalisha homoni na sumu ambazo moja kwa moja huathiri afya na tabia yako.

Aina ya mafuta yaliyo ndani ya kitambi

Lakini, kabla hatujaenda kuangazia kwa undani uhusiano wa kitambi na magonjwa mbalimbali ikiwa ni pamoja na upungufu wa nguvu za kiume ambacho ndiyo kilio cha wanaume wengi wenye vitambi, kwanza ni muhimu tufafanue kwa ufupi aina za mafuta yaliyo tumboni.

Tumboni kuna mafuta ya aina mbili. Aina ya kwanza ni mafuta yanayotokea chini ya ngozi ya tumbo. Mafuta haya unaweza kuyagusa kwa nje kwa kufinya ngozi ya tumbo. Mafuta haya hayana madhara yoyote na yana msaada mkubwa kwa viungo vilivyo ndani ya tumbo, hukaa kama mto (cushion) kwa viungo kujiegemeza. Kitabibu mafuta haya huitwa, “Subcutaneous fat.”

Aina ya pili ya mafuta, ni mafuta ambayo kitabibu huitwa, “Visceral fat,” ambayo tumekwishayataja mwanzoni mwa makala hii. Haya ni mafuta ambayo hukaa ndani kabisa ya tumbo, hujitengenezea makazi yake karibu kabisa na ini na viungo vingine viliomo tumboni. Mafuta haya ndiyo tatizo na chanzo cha matatizo mengi ya kiafya katika mwili wako, na ndiyo mafuta tunayokwenda kujadili madhara yake katika makala haya, sababu ya kutokea kwake na ufumbuzi wake.

Kisukari

Moja ya madhara ya kitambi ni kwamba, huweza kumfanya mtu apate ugonjwa wa kisukari kwa urahisi zaidi. Kwa sababu mafuta ya kitambi kwa ujumla huzonga viungo ambavyo husaidia kurekebisha sukari ndani ya damu.

Pindi insulini inapolielekeza ini kuhifadhi sukari ya akiba kwa ajili ya nishati ya baadaye, ini lililozongwa ndani tishu za mafuta hushindwa kuitikia ipasavyo. Matokeo yake, sukari huweza kuanza kujazana ndani ya mishipa ya damu na hivyo kuleta madhara makubwa katika viungo na kukaribisha ugonjwa wa kisukari.

Hali hiyo kitabibu huitwa “insulin resistance” ambapo seli za mwili hugoma kukubali homoni ya insulini. Insulini ni homoni ambayo hutolewa na seli za kongosho zijulikanazo kama beta cells. Hizi seli hutawanyika katika kongosho lote katika vishada vidogo vidogo vinavyojulikana kama visiwa (islets) vya Longerhans. Kazi kubwa za insulini huelekezwa kwenye umetaboli wa usimamizi wa kabohaidreti (sukari) na wanga, mafuta na protini.

Insulini pia hurekebisha kazi za seli za mwili, ikiwa ni pamoja na ukuaji. Insulini ni muhimu sana kwa matumizi ya mwili kama nguvu. “Insulin resistance” ni hali ambayo seli za mwili hugoma kukubaliana na insulini. Hii inaweza kuwa ni hali ya kawaida kama kiwango cha insulini kimepunguzwa. Matokeo yake viwango vikubwa vya insulini huhitajika ili insulini kufanya kazi yake vizuri. Hivyo, kongosho hufidia kwa kujaribu kutoa insulini zaidi. Mgomo huu hutokea katika mwili kuitikia insulini yake yenyewe (endogenous) au pindi insulini inapokuwa inaingizwa kwa sindano (exogenous).

Katika “insulin resistance” kongosho hutoa insulini zaidi na zaidi mpaka kufikia wakati sasa haliwezi tena kutoa insulini ya kutosha kwa ajili ya mahitaji ya mwili, hivyo sukari ndani ya damu hupanda.

Mshtuko wa moyo

​Kitambi kina urafiki mkubwa na ugonjwa wa moyo. Pindi unapokula chakula, kiwango chako cha insulini ndani ya damu hupanda. Kadiri sukari inavyopanda, ndivyo pia insulini nyingi inavyotolewa na kongosho ili kuendelea kuifanya sukari isipande juu zaidi.

Punde tu baada ya insulini kufanya kazi yake ya kushushua viwango vilivyopanda vya sukari, ini huondoa insulini kutoka ndani ya damu.

Hata hivyo, mafuta yaliyo ndani ya mikondo ya ini, huzuia na kukinza seli za ini kuondoa insulini kutoka katika mikondo ya damu.

Kwa hali hiyo, watu ambao hutunza mafuta mengi tumboni, wajue pia hutunza mafuta mengi katika ini zao, hali ambayo mafuta hayo huzuia ini kuondoa insulini ndani ya damu na hivyo kusababisha kuwa na kiwango kikubwa cha insulini.

Ni kwamba unahitaji insulini kuzuia viwango vya sukari ndani ya damu kupanda juu, lakini insulini nyingi hubana mishipa ya ateri na kusababisha mshtuko wa moyo.

Vyakula vya mafuta na ukosefu wa mazoezi husababisha ongezeko la uzito. Hali hii huzifanya njia katika mishipa ya damu kuwa miembamba zaidi na kukakamaa, matatizo ambayo hujulikana kitaalamu kama atherosclerosis au arterioscloris. Huu ni mchakato wa kunenepa na kukamaa kwa kuta za ateri kubwa na ateri za ukubwa wa kati.

“Arterioscloris” ni hali ambayo husababisha kutokea kwa maradhi ya ateri za moyo (coronary artery) ikipelekea kwenye ugonjwa wa moyo unaosababisha maumivu kifuani (angina) na mshtuko wa moyo, kupooza, na maradhi ya mishipa ya damu. Hii hutokana na lehemu (cholesterol) na baadhi ya vitu kujijenga katika kuta za mishipa ya damu.

Kama ujenzi huo wa lehemu utatokea katika mishipa mikubwa ya ateri karibu na moyo itasababisha mshtuko wa moyo, na kama itatokea katika mishipa midogo ya damu inayokwenda kwenye uume, kama tutakavyoeleza baadaye, itasababisha kushindwa kusimama kwa uume. Hali hii ya kushindwa kusimama kwa uume, kitabibu ni dalili ya tahadhari ya awali ya matatizo ya moyo.

Vipengele vinavyoweza kusababisha “arterioscloris” ni pamoja na “insulini resistance,” lehemu mbaya (LDL), shinikizo la damu la kupanda (HBP), uvutaji sigara, na kisukari.

Mshtuko wa moyo mara nyingi hutokea pindi damu inapoganda na hivyo kuziba mtiririko wa damu kupitia ateri ya moyo (coronary artery). Huu ni mshipa wa damu unaojaza damu inayokwenda sehemu za misuli ya moyo. Mtiririko wa damu ulioingiliwa unaweza kudhuru au kuharibu misuli ya moyo.

Mshtuko wa moyo pia huitwa myocardial infarction. Ni ugonjwa ambao mtu anaweza kujikuta katika hatari kubwa. Hii ni kwa sababu mara nyingi watu huchanganya dalili zake kwa kuziona ni za ugonjwa mdogo na hivyo kuchelewa kupata matibabu.

Watu wenye vitambi wako katika hatari kubwa ya kupata matatizo ya moyo kuliko watu ambao hawana vitambi.


Ni kwa namna gani kitambi huathiri nguvu za kiume?

​Tumeona hapo juu kwa ucahe jinsi kitambi kinavyoathiri afya. Sasa tuangalie jinsi kitambi kinavyoathiri nguvu za kiume.

​Mzunguko wa damu

Kitambi kinaenda bega kwa bega na upungufu wa nguvu za kiume. Kwa nini? Kwa sababu kitambi huharibu mzunguko wa adamu. Tunahitaji mzunguko wa damu wenye afya kwa ajili ya damu hiyo kuingia ndani ya uume na kujaa. Kama damu ya kutosha haingii kwenye uume nguvu za kiume pia hupotea. Uume hauwezi kusimama vizuri.

Homoni

Kibaya zaidi ni kwamba kitambi hubadilisha homoni ya kiume iitwayo testosterone kuwa homoni ya kike estrogen. Hili hutokeaje? Ni hivi. Mafuta ya kwenye kitambi huzalisha kimeg’enya kiiwatcho aromatase, na hiyo aromatase ndiyo inayobadilisha homoni ya kiume ya testosterone kuwa homoni ya kike estrogen.

Mishipa ya neva

Mafuta yaliyo kwenye kitambi hudhuru mishapa laini inayohusika na usimamaji wa uume. Uzito mdogo hata wa shilingi kutokana na mafuta yaliyo kwenye kitambi huweza kudhuru mishipa ya neva inayosimamisha uume.

Tezidume

Mafuta yaliyo kwenye kitambi pia huaharibu utendaji wa tezidume iitwayo tezidume (prostate gland) kwa sababu uzito wa mafuta hayo huleta shida kwenye tezidume.

Misuli

Pia uzito wa mafuta ya kwenye kitambi hudhuru misuli iitwayo pelvic floor muscles. Hii ni misuli muhimu sana, iko chini ya nyonga. Inafanya kazi nyingi, baadhi ya kazi zake ni kusaidia kusimamisha uume kuwa imara kabisa, na pia kuzuia kufika kileleni haraka. Mafuta ya kwenye kitambi huidhikisha misuli hii na kuipa shida.
KITAMBI KINAVYOATHIRI NGUVU ZA KIUME NA AFYA KWA UJUMLA

Monday, April 2, 2018

MADHARA YA KUJICHUA

madhara ya kujichua
Upigaji wa punyeto au kujichua hupunguza sana nguvu za kiume na hata kuua kabisa nguvu hizo za kiume. Ni jambo ovu na hatari kabisa kwa afya ya mwanaume.
 
​Moja ya sababu za kupungua nguvu za kiume kwa vijana wengi na hata baadhi ya watu wazima, ni mtindo mbaya wa kujichua au kwa lugha nyingine ‘kupiga punyeto’ tendo ambalo kwa Kiingereza linalojulikana kama masturbation. Katika makala haya, tutakuwa tunatumia majina yote matatu: kupiga punyeto, au kujichua, au masturbation.

Watu wengi hawafahamu madhara ya masturbation, hali ambayo huwasababisha wakajikuta wamedumbukia katika chama cha upungufu wa nguvu za kiume. Mbali na kusababisha upungufu wa nguvu za kiume, masturbation ina madhara mengi ya kiafya (kimwili na kisaikolojia).

Katika sehemu hii ya punyeto [masturbation], ambayo ndiyo tunaanza kufungua sababu zinazosababisha kupungua nguvu za kiume, tutatazama kwa mapana na marefu namna punyeto inavyoathiri nguvu za kiume, na pia tutatupia jicho katika madhara yake mengine ya kiafya.

Nini maana ya kupiga punyeto?

Katika kamusi nyingi za Kiswahili, punyeto huelezewa kama “Tendo la mwanamume kujipuna au kujisugua tupu ya mbele ili kutoa manii.” Hata hivyo punyeto pia hufanywa na wanawake, licha ya kwamba idadi yao ni ndogo.

Kwa ufafanuzi zaidi, kujichua au kupiga punyeto ni msisimko wa viungo vya kujamiana, ambao mara nying hufanywa na mtu mwenyewe ili kufikia mshindo wa kipeo cha raha ili kujikidhia hitaji lake la kingono.

Ingawa upigaji wa punyeto unaweza kufanywa na wote wawili (mke na mume) kwa pamoja; hata hivyo, istilahi hii mara nyingi hurejelea zaidi kujiridhisha kingono kunakofanywa na mtu mmoja.

Watu wengi sana hutumia mikono yao kupiga punyeto, lakini vifaa kama vitingishi [vibrators] n.k, vinaweza pia kutumika. Vifaa hivi hujifananisha na miondoko au mijongeo ya mikono na kumuongezea mhusika raha. Hata hivyo, njia ya mkono ndiyo maarufu sana, na ndiyo inayofanywa na watu wengi sana hususan huku kwetu Tanzania.

Hivyo, masturbation ni njia ya kuviletea msisimko wa hiari viungo vya kujamiiana ikifuatiwa kwa ujumla na utoaji wa manii kwa njia isiyokuwa ya kawaida, njia hii pia hujulikana kama ‘mtu kujiangamiza mwenyewe’ kwa sababu mtu anaitumia akili na mikono yake mwenyewe kujidhuru wakati wanawake wameumbwa kwa ajili yake, kinachotakiwa tu ni kufuata njia halali iliyowekwa na Muumbaji, MWENYEZI MUNGU.

Takriban watu wengi hasusan wanaume na hasa vijana wamefanya masturbation, yaani wamepiga mgalala. Katika kila wanaume 10 ninaowatibu nguvu za kiume, karibu watu 7 wamepiga mgalala. Tofauti pekee ni namna wanavyofanya hiyo masturbation, muda wanaotumia. Mwingine anatumia mikono tupu, mwingine sabuni, mwingine kwa kuangalia picha za uchi (kwenye gazeti au video). Mwingine anaweza kupiga punyeto miaka mitano! Mwingine miezi mitano!

Tabia hii ni moja ya sababu kubwa ya kupungua nguvu za kiume kama ambavyo tunakwenda kueleza hivi punde, na kama itafanywa sana mtu anaweza kuwa hanisi kabisa!! Masturbation huleta matatizo mengi ya kiafya katika mwili wa mtu kwa kuubana na kuukaza mwili. Mbano na mkazo huo huzalisha matatizo mengi katika moja ya njia zifuatazo: kwa kubadilisha ukubwa wa baadhi ya maeneo ya mwili; kwa kubadilisha sura za baadhi ya maeneo ya mwili; kwa kuzidhikisha baadhi ya tishu za mwili; kwa kubadilisha baadhi ya nguvu ndani ya mwili tofauti na jinsi mwili unavyofanya kazi; kwa kuvuruga na kubadilisha homoni na kemikali ndani ya mwili.

​Ni kwa kiwango gani upigaji punyeto huleta madhara?

Hakuna upigaji punyeto uliyo salama na pia vilevile hakuna kiwango kilicho salama, licha ya kwamba mtu aliyefanya aliyejichua kwa kiwango kidogo ana nafasi ndogo ya kupata madhara.

Hata hivyo, hakuna idadi maalumu inayoweza kuchukuliwa kama ni uchuaji au ufanyaji masturbation mkubwa au wa kupindukia (iliyovuka kiwango). Idadi ya kujichua (masturbation) anayoweza kufanya mtu bila madhara hutegemea afya ya mtu huyo na kemia ya mwili wake.

Baadhi ya watu hupiga punyeto (masturbation) kwa muda mfupi katika kipindi fulani, mathalani mwezi mmoja tu au miwili. Na wengine wanaweza kufanya masturbation kwa muda mrefu kiasi cha mwaka mmoja au zaidi na hata huweza kufikia mara 2 hata mara 5 kwa siku, na wanaweza kufanya kila siku (non stop)!

Kwa hakika huo ni upigaji punyeto uliyovuka mipaka, ni lazima itadhikisha ini na kazi za mfumo wa neva na lazima imweke mtu katika uhanisi hata kama ni kijana wa miaka 18, na kwa baadhi ya watu hata ugumba! Wanaume wengi sana walio na umri chini ya miaka 40 wana tatizo la kuishiwa nguvu za kiume kutokana na kujichua, yaani kupiga mgalala (masturbation).

Ni wazi kwamba watu wengi wanapokuwa wanapiga punyeto, wanakuwa hawajui wanachokifanya, kama wangelijua basi wangeliichukia punyeto kama wanavyochukia ukoma! Hata baadhi ya watu wamediriki kunitumia meseji kutaka kujua uhusiano wa upungufu wa nguvu za kiume na punyeto, makala hii ni muafaka sana kwao sasa.

Upigaji punyeto huleta mabadiliko makubwa katika mwili kama ambavyo nimeshagusia. Madhara ya mabadiliko haya ndani ya kemia ya mwili yanaweza kujidhihirisha yenyewe kama uchovu, kupoteza nywele, kupoteza kumbukumbu, kuona ukungu, maumivu ya korodani/kinena, kufika kileleni haraka, kutoka kwa shahawa zenyewe, kushindwa kusimamisha uume vizuri, kukosa uzazi, maumivu ya mgongo/kiuno n.k.

Uume kusimama kwa uregevu


​Naam! Hapa sasa tutazame madhara yanayoletwa na masturbation ndani ya mwili, tutaangaliza kwa ujumla kuhusu nguvu za kiume na vipengele vingine vya kiafya.

Kama masturbation itafanywa sana kupindukia, huchochea kemikali iitwayo acetylcholine katika mfumo wa neva huria ubongo za parasimpathetiki (parasympathetic nerve). Hali hii inaweza kuzidisha sana kupita kiasi kiwango cha mchocheo, na matokeo yake itaweza kuzalisha sana kupita kiwango cha kawaida homoni zinazohusika na kujamiiana (sex hormones) na neurotransmitters kama vile acetylcholine, dopamine, serotonin na hivyo kusababisha mabadiliko ya kemia ndani ya mwili.

Dopamine ni kemikali inayotengenezwa katika ubongo na iko katikati, na ni kipitisha ujumbe (neurotransmitter). Dopamine huhusika sana na raha. Kichocheo ambacho huzalisha aina yoyote ya mwitikio chanya pia vilevile huchochea utoaji wa dopamine katika ubongo.

Uzalishaji huu mwingi wa kupita kiasi huenda moja kwa moja kudhoofisha mfumo wa viungo vinavyoshughulika na uzazi na tendo la ndoa. Na hatari yake kubwa ni kwamba, kama mtu hatatibiwa mapema, anaweza kuua nguvu za kiume kabisa na hata kujiletea ugumba.

Parasympathetic nerve ni neva yenye jukumu la kusimamisha uume, kama mtu atafanya masturbation ya kupindukia, atazalisha kemikali nyingi ndani ya mwili, na uzalishaji huo hudhoofisha utendaji wa neva hii kwa kuifanyisha kazi kupita kiasi, na hivyo kwa baadaye uume wa mpiga punyeto unaweza kuwa unasimama kwa uregevu. Mfano wake ni kama umeme huu tunaoutumia majumbani mwetu kwa kazi mbalimbali. Pengine tukitumia mfano wa umeme, msomaji anaweza kuelewa kwa urahisi zaidi.

Ni kwamba, ndani ya miili yetu pia kuna umeme (bioelectricity). Unapofanya tendo la ndoa unazalisha umeme wa kawaida ndani ya mwili wako katika hali ya kawaida kwa sababu ni mwungano wa jinsia mbili tofauti, ni kama hasi na chanya. Lakini, unapofanya masturbation hali ni tofauti.

​Katika masturbation unazalisha umeme/kemikali nyingi sana, kwa sababu ‘unafosi’ umeme kutengenezeka kwa nguvu kwa kupitia chanya tu, umeme huo unaenda kuua vitu vinavyofanyiwa kazi na umeme huo. Ni kama ambavyo tumekuwa tukiona mara kwa mara umeme unapozidi majumbani mwetu, vitu ambavyo vilivyokuwa vikitumia umeme huo kama friji, tv, na kadhalika huungua.

Katika miili yetu hali ni hivyo hivyo. Kwa hali hiyo, wapiga punyeto, watambue wanafanya jambo baya sana, watambue wanajiangamiza kwa mikono yao wenyewe.

Madhara ya kuregea kwa uume kutokana na kujichua (masturbation), yanaweza kuanza kuonekana mapema au yanaweza kutokea baada ya muda mrefu, kutegemeana na afya ya mhusika na kemia ya mwili wake.


Kufika haraka kileleni

Upigaji wa punyeto au kujichua hupunguza sana nguvu za kiume na hata kuua kabisa nguvu hizo za kiume. Ni jambo ovu na hatari kabisa kwa afya ya mwanaume. Kudhoofika kwa neva huria ubongo za parasimpathetiki (parasympathetic nerve) husababishwa na upigaji punyeto wa kupindukia. Kama ambavyo nimekwishaeleza katika sehemu makala zingine, neva hii ndiyo yenye jukumu la kusimamisha uume, pia vilevile neva hii ndiyo yenye jukumu la kufunga milango ya shahawa kwa muda wa kutosha wa kufurahia tendo la ndoa. Pindi neva hii inapokuwa dhaifu, maji ya shahawa hutoka hata kama mtu yuko usingizini, wakati wa ndoto za mapenzi au hata wakati wa msisimko mdogo sana.

Kwa nini mtu afike kileleni mapema kutokana na punyeto? Punyeto kama lilivyo tendo la ndoa, kama ambavyo tumeshaona huzalisha baadhi ya kemikali ndani ya ubongo (acetylcholine, serotonin, na dopamine) ambazo punde tu baadaye huleta raha ya akili na mwili.

Kemikali hizi ni nzuri kwetu kwa sababu hutolewa katika kiwango maalumu. Hatari inakuja kwamba, kama zitazalishwa kwa wingi sana, zina tabia ya kukaa muda mrefu sana ndani ya mwili na kuzalisha madhara ya kimwili na kisaikololojia kama vile kutokuwa makini katika jambo, kupungua uwezo wa kukumbuka mambo, matatizo ya kukosa usingizi na mwili kukosa nguvu (physical lethargy).

Pindi mtu anapopiga punyeto sana, huchochea seli zenye jukumu la uzalishaji wa homoni hizi. Seli hizi haziitiki tu kwa kuongeza utendaji wake wa kazi, bali pia idadi yake huongezeka kuliko kawaida, na hivyo mwili wa mpiga punyeto unakuwa na msisimko mkubwa sana, kiasi ambacho hata mwanamke anaweza kuvua nguo tu, na muathirika wa punyeto akajipizia mwenyewe!

Jambo jingine baya ni kwamba, uzalishaji mwingi wa homoni hizi moja kwa moja huathiri neva ya parasimpathetiki (Parasympathetic nerve) yenye jukumu muhimu la kufunga milango ya maji ya shahawa kiasi cha mwanaume kufurahia tendo la ndoa na kuridhika na mwenza wake. Hivyo, neva hii inapoathirika, yaani inapokuwa regevu na ufikaji kileleni pia huathirika kwa kiwango kikubwa sana, kwa maana milango iko wazi, kufuli hakuna! Yaani neva inakuwa haina uwezo wa kufunga milango ya shahawa.

Madhara mengine makubwa na hatari yanayoletwa na mpiga punyeto ni kwamba, tendo hili kwa kiwango kikubwa sana hudhuru kiungo muhimu sana kwa mwanaume kinachoitwa tezi-dume au tezi-shahawa (prostate gland). Kiungo hiki kiko chini ya kibofu cha mkojo. Baadhi ya kazi zake kubwa ni kutengeneza maji ya shahawa na ‘kukontroo’ shahawa. Kiungo hiki ndicho jeuri ya mwanaume, na pia tutakizungumza tena kwa urefu katika makala zetu za mbele.

Kwa ufupi tu ni kwamba, prostate gland ndiye dreva; ndiye anayeamua kwamba hapa anafunga breki au hapana.

Tezi hii ndiyo inayoamua kuwa sasa unafika kileleni au hapana. Wapiga punyeto huzalisha umeme mwingi ambao umeme huu huifanyisha kazi sana tezi hii na hivyo kuitanusha sana, na hivyo kuvimba. Inapovimba, ugonjwa ambao kitaalamu tunauita, Benign Prostate Hyperplasia (BPH), mpiga punyeto anakuwa anapata tatizo la kufika kileleni haraka, na hata umri utapokwenda zaidi anaweza kupata tatizo la mkojo kiasi cha kuhitaji kufanyiwa upasuaji.

Pia, na kama mtu atafanya masturbation kabla ya kufikia umri wa miaka 21, ajue anajiua kabisa nguvu za kiume. Kwa sababu tezi hii katika wakati huu inakuwa katika ukuaji, inakoma kukua katika umri wa miaka 21.

Hivyo, mpiga punyeto kabla ya muda huo anakuwa anavuruga ukuaji wake na kwa hiyo kujiletea uhanisi hasa kufika kileleni haraka mnoo! Inapovimba tezi hii huwa inapata msisimko mkubwa sana na inakosa kabisa ‘kuntroo ya shahawa’ (ya udhibiti wa shahawa).

Hizo ndizo sababu zinazofanya wapiga punyeto wafike haraka sana kileleni. Wao wenyewe ni mashahidi, kilio chao kikubwa ni kufika keleleni haraka sana, ni kuingia tu na kumwaga!

Utamkuta mtu ni kijana barobaro ambaye ukimwona unaamini akifanya mapenzi atachukua dakika 30 kufika kileleni, na hata zaidi hapo, na hata mke wake atamwamkia, “Shikamoo mume wangu!”

Yaani anapewa heshima ya kipekee hata kama ana umri mdogo zaidi ya mke wake. Lakini ajabu barobaro huyu atakawambia anafika kileleni ndani ya dakika 1 au 2 au 3!! Huu tayari ni uhanisi! Hivyo mpiga punyeto aelewe kwamba anapofanya mchezo huo mchafu anaharibu milango yake ya shahawa, anadhuru tezidume, anadhuru misuli. Na hata baadhi ya wapiga punyeto uume huwa mdogo, au korodani kusinyaa na kuwa kama za mzee.

Wapiga punyeto wamekuwa wakijiuliza kwa nini baadaye wamepata tatizo la ufikaji haraka kileleni? Kwa ufupi sababu zao ni hizo, hivyo matibabu yanapaswa yaanzie katika sababu hizo. Wasikurupike tu kubugia dawa, wanahitaji wapate mtaalamu aliyebobea katika mfumo wa mkojo na mfumo wa uzazi wa mwanaume, siyo kununua dawa mitaani.

Vijana wanaosoma shule za kulala, na wanaopenda kutazama picha za ngono wana tabia hii sana ya kupiga punyeto, waelewe watakuja kukosa heshima ndani ya majumba yao punde muda tu watakapokuwa wako katika maisha ya ndoa. Waelewe watawatesa sana wake zao, kiasi hata hao wake zao kutoka ndani ya ndoa zao, ili wapate mahala pengine (kwa watu ambao hawajapiga punyeto) ili nao wastarehe na kufurahia tendo la ndoa. Kuna msemo usemao, “Usipofyeka msitu, nyoka na wanyama wabaya wataingia.”


MATIBABU ZEPHANIA LIFE HERBAL CLINIC

Zephania Life Herbal Clinic Office
Tunatibu madhara yaliyotokana na punyeto hadi mtu kupona kabisa. Pia, tunarudisha hali ya nguvu za kiume kama ilivyokuwa zamani. Ni matibabu ya uhakika na ya kitaalamu zaidi. Kinachotakiwa ni mtu kuwa na subira kipindi cha matibabu, maana matibabu haya kupona kwake huanzia mwezi mmoja hadi miezi 12 na hata zaidi ya hapo kutegemeana na uzito na ukubwa wa tatizo la mtu. Mbali na matibabu pia tunampa mwongozo wa chakula na ushauri juu ya afya yake kwa ujumla.

NINI MAANA YA KUPUNGUA NGUVU ZA KIUME?

Maana ya kupungua nguvu za kiume
Nguvu za kiume ni tukio pana sana lenye kuhusisha viungo na vitu vingi ndani ya mwili. Kuna zaidi ya viungo na vitu mbalimbali zaidi ya 100 ndani ya mwili wa mwanaume vinavyohusika na nguvu za kiume ambapo viungo hivi pia hufanya kazi zingine za mwili. Baadhi ya viungo hivyo ni ubongo, moyo, mishipa ya neva mishipa ya ateri, mirija iliyo ndani ya uume iitwayo corpora cavernosa.

Viungo vingine ni neva maalumu za parasympathetic, tezidume (prostate gland), ini, figo, homoni ya testestorone, kemikali za acetylcholine, serotonin, na dopamine, uti wa mgongo, eneo la chini ya mgongo (kiuno), eneo la nyonga.

Viungo vingine ni misuli maalumu iitwayo pelvic floor, tezi pituitari (pituitary gland), utando maalumu wa uumeni uitwao tunica albuginea, misuli iitwayo pubococcygeus [PC muscles], kemikali ya nitric oxide, kemikali ya prolactin n.k. Orodha ni ndefu sana, ni zaidi ya 100!

Unapopungua nguvu za kiume, kama nilivyosema hapo awali, ina maana ndani ya mwili wako kuna baadhi ya vitu katika vitu nilivyovitaja hapo juu havifanyi kazi vizuri jinsi ipasavyo. Yawezekana ni figo ndilo halifanyi kazi vizuri, au ini, au tezi dume, au neva ya parasympathetic, au moyo una tatizo au mishipa ya ateri, au misuli ya pelvic au homoni fulani iko juu sana au iko chini sana (hormonal imbalance), orodha ni ndefu sana. Kitendo cha baadhi ya viungo hivyo kutofanya kazi vizuri basi hapo hutokea upungufu katika nguvu za kiume. Upungufu huo unaweza kuwa ni:

1. Kukosa hamu ya mapenzi; au

2. Uume kusimama kwa uregevu; au

3. Kuwahi kufika kileleni; au

4. Kuchelewa sana kufika kileleni (au kushindwa kufika kileleni kabisa); au

5. Kushindwa kurudia tendo la ndoa; au

6. Kuhisi maumivu wakati wa tendo la ndoa au baada ya tendo hilo; au

7. Kukosa pumzi na uchangamfu wa mwili katika utendaji; au

8. Kuchoka sana baada ya tendo la ndoa na hata kukinai kabisa au hata kusikia kichefuchefu;

Ndugu msomaji, ili uelewe vizuri zaidi labda niseme kwamba, nguvu za kiume ni kiwanda; na ni zaidi ya kiwanda. Tukichukulia mfano wa kiwanda, ni kwamba ndani ya kiwanda kuna umeme, maji, madawa, watu (wafanyakazi wa kila taaluma na fani), mashine, mitambo n.k.

Ikitokea kitu kimojawapo kukosekana, mathalani umeme, au wafanyakazi wakagoma, au kukakosekana madawa muhimu au maji na kadhaa wakadha, basi bidhaa inayotarajiwa kupatikana sokoni, kwa hakika haitapatikana.

Vivyo hivyo nguvu za kiume, mathalani, ikitokea tezidume kutofanya kazi vyema, basi hapo mwanaume hatoona nguvu za kiume, zitapungua au zitaisha kabisa!

Kwa hiyo upungufu wa nguvu za kiume ni upungufu au kasoro za kiutendaji wa viungo ndani ya mwili wa mwanaume. Mwanaume yoyote anapaswa kutambua jambo hili, na siyo kukurupuka kubugia dawa tu.

MAELEZO ZAIDI BOFYA HAPA

NGUVU ZA KIUME NI NINI?

Afya
Nguvu za kiume ni jina la jumla lenye vipengele vingi ndani yake ikiwa ni pamoja na hamu ya mapenzi; kusimama kwa uume barabara; kuchelewa kufika kileleni kiasi cha kufurahia tendo la ndoa; uwezo wa kurudia tendo la ndoa kwa wakati muafaka; pumzi, wepesi na uchangamfu wa mwili katika kutenda tendo la lenyewe. Kwa ujumla vipengele vyote hivyo, ndivyo ukamilifu wa nguvu za kiume. Na ndiyo maana ya nguvu za kiume.

Kuna watu huwa hawajitambui kama wana tatizo la kuishiwa nguvu za kiume, na hatimaye tatizo huwa kubwa zaidi. Katika kitabu changu, VYAKULA VINAVYOTIBU NGUVU ZA KIUME, watu walikuwa wakipiga simu wakisema, “Mimi sina tatizo la nguvu za kiume ila tu nawahi kufika kileleni!” Wengine wakisema, “Mimi niko sawasawa tu ila nakosa hamu ya tendo la ndoa,” na kadha wakadhaa. Ukweli wa mambo ni kwamba:
  • Kama unakosa hamu ya tendo la ndoa, una tatizo la kuishiwa nguvu za kiume.
  • Kama uume hausimami barabara, una upungufu wa nguvu za kime.
  • Kama uume unasimama kwa muda mfupi na kulegea, una upungufu wa nguvu za kiume.
  • Kama uume wako hulegea muda mfupi tu baada ya kuingia ukeni, una tatizo la kuishiwa nguvu za kiume.
  • Kama unafika kileleni muda mfupi tu baada kuingia ukeni, una tatizo la kuishiwa nguvu za kiume.
  • Kama unashindwa kufika kileleni una tatizo la kuishiwa nguvu za kiume.
  • Kama unasikia maumivu wakati uume unaposimama, una tatizo la kuishiwa nguvu.
  • za kiume.
  • Kama unashindwa kutoa mbegu (shahawa), una tatizo la kuishiwa nguvu za kiume.
Iwapo moja ya matatizo hayo yatakutokea, fahamu ya kwamba, una UPUNGUFU wa nguvu za kiume, na hivyo sasa ni muda muafaka wa kutafuta matibabu sahihi bila
kuchelewa. Unapoanza kujitibu mapema kabla mambo hayajawa mabaya zaidi, unakuwa umejitengenezea fursa pana ya kupona. Lakini, chelewa chelewa…. utakuta mwana si wako!

MAELEZO ZAIDI BOFYA HAPA

TATIZO LA NGUVU ZA KIUME NI JANGA LA DUNIA

Takwimu


Leo katika zama hizi za sayansi na teknolojia, tatizo la kupungua nguvu za kiume limekuwa kubwa sana, siyo Tanzania tu, bali duniani kote.

Hapo zamani, tatizo hili lilikuwa la wazee zaidi, lakini jambo la ajabu na la kuhuzunisha leo limekuwa ni tatizo la vijana zaidi kuliko hata wazee! Utamkuta mwanaume ni kijana wa miaka 18 au 25 au 30 au 40, lakini jinsi anavyotenda tendo la ndoa ni sawa na mzee wa miaka 90 au 100!!

​Atakwambia, “Ninafika kileleni ndani ya dakika mbili,” au “Nikimaliza tendo la ndoa raundi ya kwanza, siwezi kurudia mpaka kesho yake!” Au “Uume wangu unasimama kwa uregevu sana, na nikiingia ukeni tu, unakufa (unaregea)!”

Habari kama hizo ni nyingi kwa namna tofauti tofauti na kwa watu wengi sana. Ni utitiri wa watu, vijana kwa wazee, na vijana ndiyo wakiwa wameshika usukani (wakiongoza).

Kwa bahati nzuri matatizo mengi ya nguvu za kiume yanatibika, lakini iwapo tu kama matibabu sahihi (yanayoanzia kwenye chanzo cha tatizo yatapatikana).

Hata hivyo, kwa bahati mbaya sana waathirika wengi wa nguvu za kiume wamekuwa wakikurupuka tu kubugia dawa, na hii ndiyo sababu wamekuwa hawaponi licha ya kutumia chungu ya dawa, na pia wamekuwa wakipoteza pesa nyingi bure tu kwa matibabu hayo ya kubahatisha.

Pia kutokana na tatizo hili kuwa kubwa, kila kuchapo huibuka watu wanaodai wanaweza kutibu na kumaliza tatizo kabisa. Kwenye magazeti, kwenye mabango mitaani, katika redio n.k, kuna utitiri wa matangazo juu ya tatizo hili. Lakini, kinachokata maini zaidi ni kwamba, wengi wa wataalamu hao hawajui sababu za kupungua nguvu za kiume, wala hawajui utendaji wa mwili wa binadamu. Wengi wanadhani kuishiwa au kupungua nguvu za kiume ndiyo ugonjwa wenyewe.

​Kupungua nguvu za kiume siyo ugonjwa, ni dalili ya ugonjwa. Kuna sababu zake ndani ya mwili. Sababu hizo ni nyingi mno, ni zaidi ya 100! Anatakiwa daktari mtaalamu aliyebobea katika uzazi, mifumo ya mkojo, anayelijua vizuri figo ndani na nje, ini na mifumo mingine ya mwili, ikiwa ni pamoja na kemia ya mwili. Na inatakiwa dawa iende kutibu chanzo cha tatizo.

​Jambo muhimu analopaswa mwanaume yeyote kufahamu ni kwamba, kupungua nguvu za kiume siyo ugonjwa, ni dalili ya ugonjwa. Sentensi hii ina maana gani? Twende pamoja.

SOMA ZAIDI HAPA