Hali hii imepelekea wanaume wengi kuendelea kupata shida ya upungufu wa nguvu za kiume kwa sababu ya kukosa kujua dawa sahihi ya nguvu za kiume.
Ni ukweli usiopingika kwamba wanaume wengi tangu zamani za kale wamekuwa wakitibu nguvu za kiume kwa tiba asilia. Tiba ya asili ndiyo tiba bora kabisa ya kutibu upungufu wa nguvu za kiume, kwa sababu dawa hazina madhara kabisa.
Nguvu za kiume na vyakula
Naam! Ni sahihi na kweli kabisa kwamba kitunguu saumu kina msaada mkubwa katika nguvu za kiume. Lakini kuna kosa kubwa kwenye mitandao na hata madaktari na wagonjwa wenyewe. Kwa nini?
Kwa sababu mitandao inatoa ushauri wa jumla bila kuzingatia tatizo la mgonjwa. Upungufu wa nguvu za kiume una sababu nyingi sana. Na hivyo, si kila upungufu wa nguvu za kiume utatibiwa na kitunguu saumu. Ili unielewe vizuri tazama mifano hii mitatu hapa:
Abdi kapungukiwa nguvu za kiume kwa sababu figo zake hazifanyi kazi vyema.
Peter kupungua nguvu za kiume kwa sababu moyo wake haufanyi vyema kusukuma damu.
Samwel kapungukiwa nguvu za kiume kwa sababu ana tatizo katika tezidume
Je, watu hao watatu utawapa ushauri wa kutumia kitunguu saumu?! Katika mitandao utakuta mtu kakopi na kupesti makala za watu kwamba tumia kitunguu saumu ni dawa ya upungufu wa nguvu za kiume, na hata wengine wamediriki kuiba makala zangu nyingi sana.
Na pia, kibaya zaidi maelezo juu ya namna ya kutumia vitunguu saumu hivyo hayajitoshelezi, na pia hata ni vitunguu saumu vya namna gani ni bora zaidi hawaelezi! Hali hii imewafanya watu wengi waendelee kuteseka sana.
Sasa turudi kwenye mada ya kitunguu saumu na nguvu za kiume na mfano wetu hapo juu. Kazi kubwa ya kitunguu saumu ni kusaidia mzunguko wa damu kutembea vyema na kufika mwilini kote katika kila kiungo. Kiambato kiitwacho allicin ndiyo kitu ambacho husababisha mtiririko wa damu kuongezeka.
Kama umepungukiwa nguvu za kiume kutokana na damu kutozunguka vizuri kwenda kwenye viungo vya mwili, basi kutumia kitunguu saumu ni jambo muafaka kabisa. Katika hiyo mifano yetu mitatu hapo juu utaona peter anaweza kupata msaada mkubwa wa kutatua tatizo lake la kupungua nguvu za kiume kupitia kitunguu saumu kwa sababu kitunguu saumu kimeenda kwenye tatizo husika kabisa. Lakini Abdi na Samwel wanaweza kumaliza miaka na miaka wasiweze kutatua matatizo yao. Kwa nini? Kwa sababu kuvimba kwa tezidume na figo kushindwa kufanya hakutibiwa na vitunguu saumu.
Kuhusu kiambato cha Allicin kilicho ndani ya kitunguu saumu
Allicin iligunduliwa na mtaalamu wa Kiitaliano wa Caribbean CJ Cavallito mnamo 1944, na ni mojawapo ya viambato muhimu viliomo ndani ya kitunguu saumu. Allicin kimsingi huwajibika kwa athari nyingi ikiwa ni pamoja na uwezo wake wa kuchangia matibabu ya shinikizo la damu na cholesterol ya juu, kukakamaa kwa mishipa au kuwa migumu (atherosclerosis), na kupungua kwa mishipa.
Kutokana na ukweli kwamba atherosclerosis inachangia kupungua kwa mtiririko wa damu, ni sababu ya kuchangia upungufu wa nguvu za kiume, kwa mujibu wa madaktari wa moyo. Utafiti, hata hivyo, bado haujaweka moja kwa moja uhusiano kati ya allicini katika vitunguu na matibabu ya upungufu wa nguvu za kiume.
Wakati vitunguu inakabiliana na seli nyekundu za damu katika mwili, hidrojeni sulfudi, au H2S, huzalishwa. Watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Alabama huko Birmingham walichapisha utafiti katika jarida la Mahakama ya Taifa ya Sayansi mwaka 2007 ambayo ilionyesha kuwa H2S husababisha mishipa ya damu kutanuka na kupunguza shinikizo la damu na matatizo ya moyo.
Akiongoza utafiti, Dk David Kraus, Ph.D., aliripoti katika utafiti wake kwamba matokeo haya yanatoka katika polysulfides, ambavyo ni vitu vilivyo katika kitunguu saumu ambayo husaidia uzalishaji wa H2S.
Uwezo wa vitunguu saumu wa kutanua mishipa ya damu huboresha mzunguko wa daumu, ambao kwa moja kwa moja huchangia kupunguza tatizo la upungufu wa nguvu za kiume. Ingawa matokeo haya yanatia moyo sana, utafiti zaidi unahitajika kuhusiana na uwezo wa kitunguu saumu katika kutibu upungufu wa nguvu za kiume.